Loans
NGUVU MOJA
NGUVU MOJA
Ni mikopo ya vikundi ambayo hutolewa kwa mtu mmoja mmoja (Mwanaume
au Mwanamke) anayejiunga katika kikundi cha watu watano wenye biashara
endelevu.
Sifa za Walengwa
- Wakazi wa eneo husika ambao wanaendesha na kumiliki biashara
halali ndogondogo
- Wafanyabiashara ndogondogo ambao wako tayari kujiunga kwenye
vikundi vya watu watano watano kwa ajili ya kudhaminiana.
- Wafanyabiashara ndogondogo ambao wanaelewa kuwa deni lolote
lazima lilipwe kwa kadri ya makubaliano.
- Wafanyabiashara ndogondogo ambao wapo tayari kulipa deni
pamoja na riba iliyopangwa na benki.
- Umri usiopungua miaka kumi na nane (18) – (65)
Uundaji wa vikundi
Kikundi kitaundwa kwa hiari na watu wanaofahamiana,Kuheshimiana na
kuaminiana, wanaishi jirani na ni wafanyabiashara ambao kwa hiari yao
wamekubali kuunda hicho kikundi
- Kikundi hakitaundwa na ndugu wa familia moja (baba, mama,
mke, mume, shangazi, wifi, mke mwenza nk). Iwapo wanafamilia watapenda
kujiunga basi wawe kwenye vikundi tofauti.
- Kikundi kitakuwa na watu watano watano
- Vikundi vitano hadi sita vya watu watano watano ambavyo vipo
katika kitongoji kimoja vitaunda Senta.
- Kikundi baada ya kuundwa kitasajiliwa na benki kama sharti la
kujiunga na mpango wa mkopo.
- Kila mwanakikukundi atatakiwa kulipa shillingi 5,000 za
uanachama wa mpango wa mikopo kwa wafanyabiashara ndogondogo
Sifa na Masharti kwa mkopaji
- Mkopaji lazima awe mwananchama wa kikundi cha watu watano
- Awe amehudhuria mafunzo ya mikopo yanayotolewa na Benki ya
Wananchi kwa muda wa wiki TATU ambapo kila wiki
ni siku moja na kila hiyo siku ya wiki
ni muda wa saa moja tu.
- Mkopo utatolewa kwa mwanakikundi ambaye kikundi chake na
senta yake imekubali kumdhamini na kupitisha mkopo wake.
- Mwanakikundi awe tayari kufanya marejesho ya mkopo kila wiki.
- Kabla ya kuchukua mkopo mwanakikundi lazima awe ameelewa
vizuri kiwango cha kurejesha cha kila wiki cha huo mkopo pamoja na akiba
zote za wiki.
- Mwanakikundi aelewe kuwa baada ya kurejesha mkopo ana haki ya
kupata mkopo mwingine.
- Mikopo itakuwa na vipindi vya marejesho kama
ifutavyo:
a.
Mikopo ya Miezi mitatu
b.
Mikopo ya Miezi sita
c.
Mikopo ya Miezi tisa
d.
Mikopo ya Miezi kumi na mbili
e.
Kwa mikopo ya mwanzo 200,000-350,000-500,000 marejesho yatakuwa
mwisho miezi sita.
f.
Mwanakikundi atachagua kipindi cha marejesho kwa hiari kulingana
na mzunguko wa biashara yake.
- Mkopaji lazima aweke akiba kila wiki kwa kipindi chote
cha mafunzo
ya wiki tatu za mwanzo akiwa mwanachama wa kikundi. Akiba
zinatofautiana kulingana na kiwango cha mkopo unachokopa kwa mfano mkopo
wa laki mbili (200,000/=) akiba ni 20,000=, mkopo wa laki tatu na nusu
(350,000/=) akiba ni 35,000= na mkopo wa laki tano (500,000/=) akiba ni
50,000=
- Mwanakikundi atakapochukua mkopo atapaswa kuleta marejesho
pamoja na akiba isiyopungua sh.5,000 kila wiki.
- Mkopaji lazima aweke shilingi 200 kwa wiki kwenye mfuko wa
dharura wa senta.
- Mwanakikundi aelewe kuwa akiba anayoweka ni mali yake na
dharura ya shilingi 200 ni mali ya senta.
- Kila mkopo atakaochukua, mwanakikundi atakatwa bima ya
asilimia moja pointi (1.5%) tano ambayo endapo atafariki au kupata ulemavu
wa kudumu kama kukatika mikono na miguu deni lake lote litalipwa.
- Mkopo wa pili na kuendelea utakuwa na ada ya asilimia 3 ya mkopo
uliokubaliwa. Ada zitatotelewa na mwombaji kabla ya kupewa mkopo.
Urejeshaji wa mikopo na uwekaji wa akiba
- Mikopo yote itarejeshwa na mkopaji kwa mafungu yaliyo sawa
kila wiki katika mkutano wa senta.
- Marejesho ya mkopo yatajumuisha mkopo wenyewe, riba na akiba.
- Endapo mkopaji atashindwa kuleta marejesho ya wiki,
wanakikundi itawabidi wamlipie, iwapo fedha za kikundi hazitoshi,
wanasenta itabidi warejeshe. Hiyo ndio maana ya kudhaminiana.
- Akiba ya kila mwanachama italipia deni endapo wanakikundi au
wanasenta wameshindwa kumchangia
- Kurejesha mkopo halitakuwa suala la hiari wala halina mjadala
bali ni lazima
- Marejesho yataanza mara tu pale mtu atakapochukua
mkopo.
- Mkopoji anayemaliza deni anahaki ya kukopa mkopo mwingine
katika mpangilio ufuatao:
Mzunguko wa mkopo kwa awamu |
Kiasi cha mkopo |
1 |
200,000 – 350,000-500,000 |
2 |
800,000 |
3 |
1,000,000 |
4 |
1,500,000 |
5 |
2,000,000 |
6 |
3,000,000 |
7 |
4,000,000 |
8 |
5,000,000 |
Muhimu: Mwanakikundi anaweza kuchukua mkopo wa mzunguko wa nyuma
kulingana na hali ya biashara kadri anavyoiona na baadae anaweza kurudi katika
mzunguko wake wa kawaida hali ya biashara ikiwa nzuri tena.
Matumizi ya fedha za mkopo
Mikopo yote itatolewa kwa ajili ya kuimarisha na kukuza biashara
ya mkopaji
- Kutumia mkopo nje ya biashara ni kukiuka maadili ya mkopo
- Wanakikundi watatakiwa kuhakikisha kuwa waliyemdhamini
anatumia mkopo kuimarisha au kukuza biashara ili wasiwe na mzigo wa
kumlipia deni endapo atashindwa kurejesha.
Kujitoa kwenye mpango au kikundi
kujitoa ni hiari
- Kabla mwanakikundi hajaamua kujitoa ahahakishe madeni yote
yamerejeshwa
- Endapo wanakikundi wataona mwenzao hafai wanahaki ya
kumfukuza lakini kabla hawajafanya hivyo, madeni yote yawe yamerejeshwa.
- Mwanakikundi kama atakuwa amefukuzwa na wanakundi wenzake benki
haitatoa huduma yoyote kwake kwani huduma zote zitapitia kwenye vikundi.
Zingatia: Lengo kuu la benki ni kuona biashara ndogondogo zinakua na
kuwasaidia walengwa.
Mkopo lazima urejeshwe hapatakuwa na sababu
yoyote itakayokubaliwa kutokulipa deni.