7:06 AM
Benki ya Biashara ya DCB yaingia kwenye mizania ya kati na yajiimarisha kwa kuendelea kupata faida zaidi mwaka 2022 huku amana na mali zikiongezeka.
Benki ya Biashara ya DCB imepatafaida kwa kiwangokikubwa kwa mwaka wa fedha wa 2022 ukilinganisha na faidailiyopatikana kwa kipindikamahichomwaka2021 hukumali za benkihiyo na amanazikiongezeka.
11:08 PM
DCB Bank yakutana na Wizara ya Maji
Benki ya DCB, ikiongozwa na Sabasaba Moshingi – Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara DCB, imetembelea ofisi za Wizara ya Maji jijini Dodoma na kufanya mazungumzo na Eng. Mwajuma Waziri – Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
Tunaendelea kujenga ushirikiano wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
9:08 PM
DCB yakutana na wateja wake Dodoma
Jana, Benki ya DCB ilifanya Customer Forum jijini Dodoma, tukikutana na wateja wetu kwa ajili ya kuongeza mahusiano, kusikiliza maoni yao na kujadili namna bora ya kuboresha huduma zetu.
Mkutano huu uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Sabasaba Moshingi, ambapo washiriki walipata nafasi ya kushirikiana moja kwa moja na uongozi wa benki.
Kwa DCB, mafanikio yetu ni matokeo ya kuwa karibu na wateja wetu — kuwasikiliza, kushirikiana nao na kutafuta suluhisho pamoja.
1:00 PM
DCB Benki Yazindua Kampeni “Kwa Ground Na Wenyewe”
DCB Yazindua Kampeni “Kwa Ground Na Wenyewe” – Huduma Bure, Malipo Fasta na Gharama Nafuu kwa Wateja
Dar es Salaam, Tanzania – 7 Oktoba 2025
DCB Commercial Bank Plc imezindua kampeni yake mpya “Kwa Ground Na Wenyewe”, ikilenga kutoa huduma nafuu, za kidigitali na zenye urahisi kwa Watanzania. Kampeni hii inalenga kuwafikia wateja wa kada mbalimbali ikiwemo mama lishe, bodaboda, vijana, vikundi vya VICOBA na wafanyabiashara wadogo.
Kupitia huduma kama kutuma pesa bure, DCB Lipa FASTA kwa QR na TILL bila gharama, na kufungua akaunti kiganjani, benki inalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza gharama kwa wateja.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mikopo Bwana Deogratius Thadei, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bwana Sabasaba Moshingi, lengo la kampeni hii ni kuwa benki ya jamii inayowasaidia wateja “kwa ground” kupitia huduma za kidigitali zinazoboresha maisha na biashara zao.
Kampeni hii inalenga kukuza tabia ya kuweka akiba, kuvutia wateja wapya, kupunguza utegemezi wa pesa taslimu na kusaidia wafanyabiashara wadogo kuongeza uwazi na ufanisi wa miamala yao.
Kwa Ground Na Wenyewe – Ndio mpango mzima wa benki ya mtaa wako.