MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WANAHISA WA DCB BANK PLC (AGM) 2026
  • When
    June 26, 2026 , 12:09 PM

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WANAHISA WA DCB BANK PLC (AGM) 2026

26 Juni 2026

Mnamo tarehe 26 Juni 2026, DCB Bank PLC ilifanikiwa kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa (AGM) 2026, uliowakutanisha wanahisa, Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, wadau mbalimbali na mamlaka za usimamizi kwa ajili ya kupitia utendaji wa Benki, kujadili maazimio muhimu na kuweka mwelekeo wa maendeleo ya Benki kwa siku zijazo.

Mkutano huo ulikuwa fursa muhimu ya kuwasilisha taarifa za utendaji wa kifedha na kiutendaji wa Benki, kuimarisha misingi ya utawala bora, uwazi na uwajibikaji, pamoja na kuthibitisha dhamira ya DCB Bank PLC ya kuendelea kutoa huduma bora za kifedha zenye ubunifu na zinazokidhi mahitaji ya wateja.

DCB Bank PLC inaendelea kujenga thamani endelevu kwa wanahisa wake, kuendeleza ujumuishi wa kifedha, na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia huduma za kibenki zinazowafikia watu binafsi, biashara na jamii kwa ujumla.

Get Help from Our Chatbot
x
ChatBot
Hi 👋! welcome to DCB Chatbot
Powered by The Bridge
This chat session has ended

Thank you for chatting with us, If you can take a minute and rate this chat:

Great
Bad