Limited Company Account

Akaunti ya Hundi kutoka DCB ni mahsusi kwa ajili ya mahitaji ya wateja wakubwa na wa kati!

Akaunti ya Shilingi / Local Currency Account       Fedha za kigeni / Foreign Currency Account
Sifa na manufaa ya akaunti hii ni:

» Kiwango kidogo cha kufungua akaunti: Unahitaji Sh. 200,000 tu kufungua akaunti hii. 

» Utapata riba kwa mwezi kama utakuwa na kiwango kikubwa cha fedha katika akaunti yako au kama utajiunga na akaunti ya Call. (Call Account)
» Utapatiwa kitabu cha hundi kukurahisishia kufanya malipo.
» Urahisi wa kufanya malipo kwa kutumia hundi kwa hiyo huitaji kubeba fedha taslimu.
» Kuweza kutumia akaunti ya hundi kuomba mkopo wa muda mfupi au wa dharura (overdraft facility).
» Uhuru wa kuweka na kutoa fedha kadri uwezavyo bure katika tawi lolote la DCB.
» Fursa ya kupata ATM kadi ya UmojaSwitch, yenye mtandao wa mabenki zaidi ya 25 nchini, DCB ikiwa ni mwanachama.
» Urahisi wa kupata mkopo kwa kutumia amana yako kama dhamana.

Viambatanisho vinavyohitajika kwa ajili ya kufungua Akaunti:
- Vielelezo vya kudhibitisha biashara husika, muhtasari ya idhini ya kufungua akaunti na hati za usajili kutoka mamlaka husika
- Pasipoti, kitambulisho cha kupiga kura, leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi kwa wamiliki na watia saini.
- Picha mbili za paspoti za rangi.
- Uthibitisho wa sehemu wanayoishi wamiliki na watia saini: Mojawapo ya vifuatavyo; barua kutoka serikali za mitaa, Mwanasheria, Hati ya nyumba, Mkataba wa kupanga nyumba au bili ya umeme au maji yenye anwani ya mahali unapoishi.
 
Fungua akaunti yako ya akiba kutoka DCB sasa unufaike!

  Sifa na manufaa ya akaunti hii ni:

» Kiwango kidogo cha kufungua akaunti: Unahitaji USD/EURO/GBP 200 tu kufungua akaunti hii 
» Utapata riba kwa mwezi kama utakuwa na kiwango kikubwa cha fedha katika akaunti yako au kama utajiunga na akaunti ya Call. (Call Account)
» Utapatiwa kitabu cha hundi kukurahisishia kufanya malipo.
» Urahisi wa kufanya malipo kwa kutumia hundi kwa hiyo huitaji kubeba fedha taslimu.
» Kuweza kutumia akaunti ya hundi kuomba mkopo wa muda mfupi au wa dharura (overdraft facility).
» Uhuru wa kuweka na kutoa fedha kadri uwezavyo bure katika tawi lolote la DCB.
» Urahisi wa kupata mkopo kwa kutumia amana yako kama dhamana.

Viambatanisho vinavyohitajika kwa ajili ya kufungua Akaunti:
- Vielelezo vya kudhibitisha biashara husika, muhtasari ya idhini ya kufungua akaunti na hati za usajili kutoka mamlaka husika
- Pasipoti, kitambulisho cha kupiga kura, leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi kwa wamiliki na watia saini.
- Picha mbili za paspoti za rangi.
- Uthibitisho wa sehemu wanayoishi wamiliki na watia saini: Mojawapo ya vifuatavyo; barua kutoka serikali za mitaa, Mwanasheria, Hati ya nyumba, Mkataba wa kupanga nyumba au bili ya umeme au maji yenye anwani ya mahali unapoishi.Fungua akaunti yako ya akiba kutoka DCB sasa unufaike!